loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uganda yang’ara Afcon

TIMU ya taifa ya Uganda ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 `Uganda Hippos’ imetinga robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika, Afcon 2021 nchini hapa mwishoni mwa wiki.

Uganda ilijihakikishia nafasi hiyo baada ya kuwachapa wenyeji Mauritania kwa mabao 2-1 katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi.

Ushindi huo una maana kuwa Uganda imemaliza katika nafasi ya pili katika Kundi A ikiwa nyuma ya Cameroon ambayo ilipata pointi zote katika kundi hilo.

Uganda ikicheza kwa ari kubwa ilipambana na kupata mabao mawili katika kipindi cha pili likiwamo la ushindi lililofungwa dakika za mwisho kabisa za mchezo huo.

Mabingwa hao wa Cecafa kwa U-20 walienda mapumziko wakiwa nyuma baada ya wenyeji kufunga bao la kuongoza na matokeo kuwa 1-0 kwa bao lililofungwa na Silly Singhare.

Alifunga kwa penalti baada ya Aziz Kayondo kumuangusha Oumar Mbareck katika eneo la hatari.

 

Singhare alipiga kifundi penalti hiyo na kumuacha kipa Jack Komakech akienda sehemu tofauti na mpira ulipokwenda na kuiwezesha Mauritania kuongoza dakika tano kabla ya mapumziko.

Hata hivyo, Uganda ilirejea kwa nguvu kutoka katika mapumziko na kufanya mashambulizi kadhaa hadi pale jitihada zao zilipozaa matunda.

Sserwadda ambaye mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwake kuanza, alifunga baada ya kupata pasi kutoka kwa Sam Ssenyonjo na kumpatia mfungaji aliyefunga kwa shuti la karibu.

Hili ni bao lake la pili katika mashindano hayo, huku jingine alifunga walipocheza dhidi ya timu ya taifa ya Msumbiji alipoingia akitokea benchi.

Dakika mbili kabla ya mchezo kumalizika, Uganda ilizawadiwa penalti baada ya beki Mohamed Sarr kuukamata mpira ndani ya eneo la hatari.

KOCHA Mkuu wa miamba ya soka Tanzania, Didier ...

foto
Mwandishi: NOUAKCHOTT, Mauritania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi