Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato amewahakikishia umeme wa kutosha sambamba na kuongeza nishati hiyo kwa wawekezaji wa Sekta ya Madini wenye nia ya dhati ya kuwekeza katika Mkoa wa Singida.
Akizungumza leo katika Mkutano wa Uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Singida, Byabato amesema licha uwepo wa umeme wa kutosha, lakini Serikali kwa kushirikana na wizara hiyo iko katika hatua za mwisho za kutengeneza transfoma yenye uwezo wa kuzalisha megawatt 100.
“Kwahyo tutatoka kwenye Megawati 132 hadi 232, na tukitumia hizo kumi ambazo zinatumika kwasasa kwa mkoa mzima, tunabakiza megawatt zaidi ya 220, umeme ule ni wa gridi ya Taifa na unakuja katika msongo wa kilovolt 220, kwahyo ni umeme mkubwa wa kutosha kabisa.”amesema Byabato.
Amefafanua kuwa kwa matumizi ya mkoa wa singida, mpaka sasa wanatumia megawatt 10.7 lakini kituo cha kupoza umeme kina uwezo kutoa megawatt 132 hivyo kuna megawatt 122 zisizotumika.