loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Vifo 500,000 vyampa mawazo Biden

RAIS wa Marekani, Joe Biden amelihutubia taifa baada ya kufikisha vifo zaidi ya 500,000 vinavyotokana na ugonjwa wa Corona, idadiambayo haijafikiwa na nchi yoyote duniani.


Biden amewataka wamarekani kutokubali na hali hiyo na badala yake wapambane dhidi ya Covid-19.


Rais huyo, Makamu wake pamoja na wenza zao, walishiriki uwashaji mishumaa nje ya Ikulu ikiwa kama ishara ya kuwakumbuka wapendwa wao waliotangulia kutokana na ugonjwa huo.


Aidha, Rais Biden ametoa wito kwa watu wake kuwakumbuka wale waliopoteza maisha na waliochwa nyuma na kuwataka kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.


Hadi sasa idadi ya maambikizi katika taifa hilo yamefikia milioni  28.1.

Makamu wa Rais wa Zimbabwe, Kembo ...

foto
Mwandishi: WASHNGTON, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi