Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Mwigulu Nchemba amesema kuwa ukomo wa mtu kukaa ndani ni saa 24 lakini mabadiliko yanaweza kutokea iwapo usalama wa mtu anayeshikiliwa ukawa mdogo kama akitoka nje.
Mwigulu amebainisha hayo leo Jijini Dar es Salaam ambapo amebainisha kuwa vitu hivyo vinaweza kufanyika kwa ajili ya kumlinda mhusika au mtuhumiwa.
“Chukulia mfano mtu kabaka na watu wameshuhudia akawekwa ndani halafu ndani ya saa sita akatoka yule mtu lazima atadhurika hivyo vitu hivi vimewekwa si kwa ajili ya kumuadhibu mtu bali kupunguza hasira ya wale waliokosewa,” amesema Nchemba.
Aidha, Nchemba amevihimiza vyombo vinavyosimamia haki kutimiza wajibu wao ipasavyo haki ionekane ikitendeka ili kuepusha wananchi kujichukulia sheria mkononi.