loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ronaldo aipa uhai Juventus

CRISTIANO Ronaldo alifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 wa timu yake ya Juventus dhidi ya Crotone.

Katika mechi hiyo iliyochezwa nyumbani Turin, kikosi hicho kimeweka hai matumaini ya mbio za ubingwa. 

Juventus ilikuwa kwenye hali mbaya baada ya kufungwa na Napoli kabla ya kufungwa kwenye Ligi ya Mbaingwa dhidi ya Porto, lakini mabingwa hao watetezi walishinda juzi na kukwea mpaka nafasi ya tatu kwenye msimamo. 

Kikosi hicho cha Andrea Pirlo sasa kipo nyuma kwa pointI nane dhidi ya vinara Inter Milan wakiwa na mechi mkononi. 

Wenyeji walitawala sehemu kubwa ya mchezo katika kipindi cha kwanza lakini walisubiri mpaka dakika ya 38 kuandika bao la kuongoza lililofungwa na Ronaldo akiunganisha krosi ya Alex Sandro.

Mshindi huyo mara tano wa Ballon d'or aliongeza bao la pili kabla ya mapumziko. 

Ronaldo anaongoza orodha ya wafungaji kwenye Serie A baada ya kufunga mabao 18.

Weston McKennie alifunga bao la tatu dakika ya 66 baada ya Crotone kushindwa kuokoa mpira wa kona. 

KOCHA wa timu ya taifa ya Rwanda, Amavubi, ...

foto
Mwandishi: TURIN, Juventus

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi