loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shehe akemea wanaotumia dini kukataa vitakasa mikono

SHEHE wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu amekemea baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wanaokataa kutumia vitakasa mikono kwa madai kuwa havina tofauti na vilevi.

Kiongozi huyo wa dini alisema hayo wakati alipokuwa akitoa mawaidha kwenye Msikiti wa Gadafi uliopo Jijini Dodoma.

Shehe Rajabu alisema kumekuwepo na baadhi ya waumini wanaovumisha kuwa vitakasa mikono vinavyotumika kwa ajili ya kujilinda na maambukizi ya magonjwa ikiwemo virusi vya corona havifai kutumiwa kwa madai kuwa vina kilevi ndani yake na kwa waumini wa dini ya Kiislamu ni haramu.

Alisema katika kipindi ambacho dunia inaendelea kupambana na virusi vya corona ni lazima kuendelea kuchukua tahadhari na kuendelea kufuata mwongozo unayotolewa na Wizara ya Afya.

"Ndugu zangu Waislamu tupo katika kipindi cha mapambano dhidi ya corona, kutokana na hali hiyo tuendelee kuchukua tahadhari ya kiafya, tuvae barakoa, tunawe mikono na kutumia vitakasa mikono huku tukimuomba Mungu kwa kila wakati...

"Kuna watu ambao wanasambaza uvumi na uzushi kwa kueleza kuwa vitakasa mikono vina kilevi ndani yake hivyo si sawa kwa kutumiwa, watu hao kwa kweli wanaonekana na wao waenezaji wa magonjwa haya.

"Hivyo mimi kama kiongozi wenu ninawasihi waumini na watanzania kwa ujumla maneno hayo yapuuzeni kwani tayari kiwango cha kilevi iliyotengeneza vitakasa mikono haipo katika viwango vya pombe kama vile bia au konyagi, tayari matumizi yake ni mengine kabisa.

"Ebu jiulize hapa wote tunavaa viatu na mikanda na hiyo ni ngozi lakini unajua hiyo ngozi imepatikanaje? Je unajua nani alichinja au mnyama alijifia alikuwa kibudu, kwa maana hiyo tuendelee na tahadhari kadri tunavyoelekezwa na serikali pamoja na wataalamu wa afya"alisema.

Akiwahimiza waumini wa dini ya kiislamu kuhakikisha wanamcha Mungu kwa kufanya mambo mema kutokana na maelekezo ya dini ya Kiislamu.

MAMLAKA ya Mawasiliano (TCRA), imezitaka kampuni za simu ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi