loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shetta akemea rushwa ya ngono

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nurdin Bilal ‘Shetta’ amesema wasanii wengi wa kike wanapitia changamoto za rushwa ya ngono ili wapate kitu jambo ambalo ni sawa na ukatili.

Akizungumza Dar es Salaam jana, nyota huyo alisema wanaofanya hivyo sio vyema na kukemea vitendo hivyo kwa kwani ni kosa la jinai.

Alisema suala hilo sio tu linawakuta wasanii wa kike bali hata wanawake walioko kwenye kazi na hata katika mihangaiko ya shughuli mbalimbali.

“Kuna vitu vinafanyika kwa watoto wa kike sio vizuri na vinafanywa na washkaji zetu, wadau, ma-Dj na watu mbalimbali na havitokei tu kwenye muziki hata kwingine.” 

“Leo hii mtu anapeleka wimbo ili upigwe labda aombwe kitu kwanza ndio apate msaada,” alisema.

Shetta alisema wana shirika lao linaitwa Sawa, ambapo wamekuwa wakifuatilia ripoti kadhaa hasa kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kugundua wasichana wengi wanapitia ukatili wa kingono. 

KOCHA Mkuu wa miamba ya soka Tanzania, Didier ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi