loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Magufuli azindua Daraja la Kijazi

Rais Dk John Magufuli leo amezindua Daraja la Juu la Kijazi lililokuwa linaitwa ‘Daraja la Juu la Ubungo'na kusema kuwa ameamua kuliita hivyo kutokana na mambo makubwa aliyofanya Balozi Kijazi katika sekta ya barabara.


Akizungumza katika uzinduzi wa daraja hilo hii leo Ubungo jijini Dar es Salaam, Dk Magufuli aliwashukuru wakazi wa mkoa huo kwa kukubali daraja hilo kuitwa jina hilo kwakuwa marehemu Balozi Kijazi alifanya kazi yake kwa uadilifu mkubwa.


“Miradi hii yote nchini hata ya Dar es Salaam ya masoko, stendi na kadhalika ilifanyika kupitia yeye kwakuwa alikuwa ndiye kiongozi wa Baraza la Makatibu Wakuu (MTC) kwahiyo kwa namna moja au nyingine amechangia kwa kiasi kikubwa kufanikiwa kwa miradi hii” amesema Dk Magufuli.


Aidha, Dk Magufuli amesema kuwa amefarijika kuzindua daraja hilo likiwa na jina la Balozi Kijazi kama kumbukumbu ya muda wote.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi