loader
Rais Magufuli atoa angalizo Mamlaka ya Mapato

Rais Magufuli atoa angalizo Mamlaka ya Mapato

Rais Dk John Magufuli ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuacha kufanya makadirio makubwa ya kodi tofauti na uhalisia kwa wafanyabiashara jambo linalopeleka muda mwingine kufunga biashara zao au kukwepa kodi.
 
Dk Magufuli amebainisha hayo  leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa anaongea na wananchi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kuitaka TRA kujifunza kutoa haki kwa wafanyabiashara ambao wana nia nzuri ya kulipa kodi.
 
Aidha, Dk Magufuli amekemea tabia ya baadhi ya wafanyabiashra wasiokuwa waaminifu kuwatumia wamachinga kuuza bidhaa zao ili kukwepa kodi.
 
“Mfanyabiashara anakuwa na stoo anapeleka biashara zake mtaani lakini anayefanya biashara hiyo sio kweli mmachinga bali mali ile imetolewa na mtu mwenye biashara kubwa naomba tabia hiyo ikome” amesema Dk Magufuli.

Katika hatu nyingine Dk Magufuli amemtaka mkandarasi anayejenga Soko la Kisutu jijini humo kuhakikisha anamaliza kazi kwa wakati katika tarehe mpya alizopangiwa kwakuwa ujenzi wa soko hilo ulitakiwa kukamilika toka mwaka jana.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/685acaed9b833a1c048a245fe0212c4e.jpg

MWENGE wa Uhuru unaendelea ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

1 Comments

  • avatar
    Paul Kapusi
    25/02/2021

    Kwanini waziri wa biashara hazunguki nchi nzima kuongea na wafanya biashara ili kubaini mapungufu?

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi