loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rais Magufuli ampa siku 7 Simbachawene

Rais Magufuli ampa siku 7 Simbachawene

Rais John Pombe Magufuli amempa siku saba Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene, ahakikishe wastaafu wote wa jeshi la polisi wanaodai mafao yao wanalipwa.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo aliposhiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa ofisi na madarasa katika Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo Kurasini mkoani Dar es Salaam.  

Rais amebainisha kuwa wastaafu hao walikuwa wazalendo kwa taifa hadi kufikia hatua ya kuhatarisha maisha yao pindi walipokuwa wanapambana na wahalifu hivyo Waziri ahakikishe wanapata mafao yao haraka.

“Kutopata mafao ni tatizo la wakubwa wenu wizarani kama mpo hapa wastaafu mumlaumu Waziri mwenye dhamana na watendaji wake huo ndio ukweli wakitaka wastaafu kulipwa watalipwa tena haiwezi kuchukua hata siku tano kama watakuwa na mawasiliano mazuri na Wizara ya Fedha,” amesema Rais Magufuli.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli ametoa ahadi ya kukipa chuo hicho kiasi cha shilingi 500 kwa ajili ya ujezi wa hospitali ili maaskari pamoja na familia zao wapate kutibiwa.

“Nimefikiria wakati nimekaa hapo kuna ubaya gani kujenga vituo vya afya katika taasisi za majeshi yetu ili maaskari pamoja na familia zao wawe wanatibiwa hapo kwa hiyo nimeamua tena kuwaletea milioni 500 zijenge hospitali kubwa hapa,“  amesema Rais Magufuli.

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge 

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi