loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rais Magufuli ahitimisha ziara, atoa maagizo kwa Jeshi la Polisi

Rais Magufuli ahitimisha ziara, atoa maagizo kwa Jeshi la Polisi

Rais John Pombe Magufuli leo amehitimisha ziara yake ya siku tatu mkoani Dar es Salaam  na kulitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha linawadhibiti wahalifu wanaotumia silaha ambao wakitoka vifungoni  hawataki kubadilika.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo aliposhiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa ofisi na madarasa katika Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo Kurasini mkoani Dar es Salaam.

“Muheshimiwa IGP umezungumza kuhusu hao wafungwa wa uhalifu mbalimbali wa kutumia silaha ambao wakifungwa wakirudi wanaendelea kurudia matukio hawataki kuyaacha, kama alikuwa jambazi anaendelea na ujambazi muwalazimishe sasa wayaache kwa nguvu na hilo najua halitakushindwa IGP” amesema Rais Magufuli.

Awali akizungumza katika tukio hilo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ,IGP Simon Sirro amewaonya watu wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu hasa wa kutumia silaha wasiilaumu Serikali pindi  jeshi hilo litakapochukua hatua stahiki dhidi yao.

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi