loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Barabara kuelekea kaburi la Dk Omari Ali Juma kukarabatiwa

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imesema itaifanyia ukarabati barabara yenye urefu wa kilomita moja kuelekea katika maeneo ya makaburi ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, marehemu Dk Omar Ali Juma, ili kuwaenzi viongozi wakuu wa serikali kwa mujibu wa sheria.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Dk Khalid Salum Mohamed, wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi lililopo Pemba, Bakari Hamad Bakari, aliyetaka kujuwa ni lini barabara ya kuelekea katika makaburi ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Muungano, Dk Omar Ali Juma itafanyiwa ukarabati.

Alisema SMZ imepitisha sheria ya kuwaenzi viongozi wakuu wa serikali inayolenga kutunza kumbukumbu mbalimbali za viongozi wakuu wa nchi.

Kwa mujibu wa waziri huyo katika SMZ, enzi za uhai wake, Dk Omar Ali Juma, alitoa mchango mkubwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kwamba, ataendelea kukumbukwa kwa mchango wake katika utumishi hata alipokuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1988 hadi 1995.

“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tumepitisha sheria ya kuwaenzi viongozi wakuu wa serikali wa kitaifa ambapo utekelezaji wake unafanyika kwa mujibu wa sheria... Barabara inayoelekea katika makaburi ya kiongozi wetu, Dk Omar Ali Juma itafanyiwa ukarabati,” alisema Dk Khalid.

Dk Omar Ali Juma alitumikia wadhifa wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu mwaka 1995 chini ya Rais Benjamin Mkapa (marehemu) hadi mauti yalipomfika Julai 4, 2001 na Mkapa kumteua Dk Ali Mohammed Shein kushika wadhifa huo.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi