loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DC ataka vijana kujenga vyoo vya kulipia

Mkuu wa Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, Klaudia Kita amewataka wananchi waishio jirani na fukwe za Ziwa Nyasa, hasa vijana, kuwekeza miradi ya vyoo vya kulipia ili kujiingizia kipato kutoka kwa watalii, wanaokwenda kwenye fukwe hizo kwa mapumziko.

Kita alitoa ushauri huo alipozungumza na wafanyabiashara wa soko la samaki lililopo ufukwe wa Ziwa Nyasa Kitongoji cha Liulilo Kijiji cha Bukombe akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila.

Mkuu wa wilaya alisema hayo baada ya baadhi ya wananchi kulalamikia ukosefu wa vyoo bora, kuwa umesababisha wageni kushindwa kupata huduma wanapokuwa kijijini hapo. Hivyo, waliiomba serikali kujenga vyoo bora.

Kita aliwaeleza wakazi hao kuwa hawapaswi kuendelea kulalamika, badala yake watumie changamoto hiyo kama fursa ya kuwekeza, kwa kujenga vyoo vya kulipia, hivyo kujiingizia kipato.

Aliwataka wasiiachie serikali ifanye kila kitu, bali wajiongeze na kuzigeuza changamoto zilizopo kwenye maeneo yao kuwa fursa zenye kuleta mabadiliko ya kiuchumi.

“Tusiache kila mradi ufanywe na serikali. Ninyi wenyewe hasa vijana undeni vikundi, tengenezeni mradi wa choo cha kulipia kwaajili ya wageni wanaokuja hapa, muwe mnawatoza, mtajipatia fedha. Vijana changamkieni fursa hii kwa kuwa pia mna nafasi ya kukopeshwa na halmashauri mkiunda vikundi,” alisema mkuu huyo wa wilaya.

Mkuu wa Mkoa, Chalamila aliwasihi wakazi wa kijiji hicho kutunza mazingira ya safu ya milima ya Livingstone iliyopo jirani. Alisema kuendelea kuharibu mazingira hayo, kutasababisha maporomoko ya ardhi yatakayohatarisha makazi na maisha yao.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Joachim Nyambo, Kyela

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi