loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Madereva wahimizwa kufuata sheria

MADEREVA nchini wametakiwa kujiamini na kuchukua tahadhari wakiwa barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika, zinazochangia maafa makubwa.

Wito huo umetolewa na Ofisa Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Mkoani Tabora, Hamisi Mshihiri aliyemwakilisha Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa Mkoa, Gabriel Chiguma.

Alisema hayo katika hafla ya kuwatunu vyeti madereva 14 waliohitimu mafunzo yao. Sherehe hiyo ilifanyika ukumbi wa Jeshi la Polisi mjini hapa.

Mshihiri alisema kuwa taaluma waliyopata wahitimu hao ni nyeti, inayohitaji umakini, weledi na busara zaidi ili kupambana na changamoto zote zinazojitokeza katika kazi zao, kwa kuwa wanabeba roho za watu.

Alisisitiza kuwa wanapaswa kuwa wepesi na kuwa waungwana wakiwa barabarani. Hata kama sheria itakuwa inawaruhusu, wanatakiwa kuwa waangalifu zaidi na kutumia busara ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea na kusababisha uharibifu na maafa.

Aliwataka kufuata sheria za usalama barabarani, kutii bila kushurutishwa na kutokuwa chanzo cha migogoro. Aliwataka kabla ya kuanza safari, wahakikishe kwenye magari yao wanakagua maji, mafuta ya vilainishi, nati, matairi na mambo mengine muhimu  waliyofundishwa ili kuondokana na ajali zinazoweza kutokea.

Aliwataka wakawe mabalozi wazuri kwa wenzao ambao sio madereva na wawashawishi wapate mafunzo. Pia aliwataka wawe na nidhamu bora, itakayokuwa kivutio kwa watu wengine wakiwemo abiria wao.

Akisoma risala kwa mgeni rasmi, Mratibu wa Mafunzo wa Chuo Cha Ufundi Arusha, David Mtunguja alisema kuwa chuo hicho kwa kushirikiana na Chuo cha Mafunzo ya Udereva cha Magu mjini Tabora chini ya Mkuu wa Chuo hicho, Charles Makungu wametoa mafunzo kwa wahitimu hao 14.

Mtunguja alisema kuwa wahitimu hao, wamehitimu katika udereva wa magari ya abiria au usafiri wa umma na magari ya viongozi. Chuo hicho kinatoa mafunzo katika nyanja mbalimbali za uhandisi kuanzia ngazi ya cheti hadi shahada ya kwanza.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Tabora

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi