loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Sumbawanga wapitisha bil 31.5/- bajeti 2020/21

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa wamepitisha mapendekezo ya bajeti ya zaidi ya Sh bilioni 31.5 kwa mwaka wa fedha 2020/21.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Nyangi Msemakweli, alibainisha hayo wakati akiwasilisha mapendekezo ya bajeti hiyo katika Baraza la Madiwani lililoketi hivi karibuni katika Mji Mdogo wa Laela walipoijadili na kuipitisha.

Akizungumzia umbile la bajeti hiyo, Msemakweli alisema halmashauri hiyo inakisia kukusanya, kupokea na kutumia Sh 31,545,302,988.51.

Alisema kati ya hizo, Sh 28,852,090,988.51 ni ruzuku kutoka Serikali Kuu. Mishahara ya watumishi ni Sh 19,186,732,000 huku ruzuku ya maendeleo ni Sh 8,480,203,988 .

“Halmashauri imekadiria kukusanya Sh 2, 693,212,000 kutoka vyanzo vya ndani katika mwaka wa fedha 2021/22.  Pamoja na miradi itakayotekelezwa kutokana na ukomo wa bajeti uliotolewa, maombi maalumu ya Sh bilioni 2, yamewasilishwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ili kuendeleza ujenzi wa kituo cha mabasi... kitakuwa chanzo cha uhakika cha makusanyo ya mapato ya ndani na kuondokana na utegemezi wa ruzuku kutoka Serikali Kuu,” alisisitiza.

Alisema changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa bajeti ni gharama za mtihani wa taifa kwa shule za sekondari.

Msemakweli alifafanua kuwa kutokana na mwongozo wa uendeshaji wa mitihani ya upimaji wa kidato cha pili (FTNA), mtihani wa kidato cha mne (CSEE) na ule wa kidato cha sita (ACSEE), ukomo wa bajeti uliotolewa ni mdogo ukilinganishwa na hali halisi.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Apolinary Macheta, aliwataka madiwani kusimamia kwa umakini mkubwa makusanyo ya mapato ya ndani katika kata zao sambamba na kubuni vyanzo vipya vya mapato badala ya kutegemea ushuru wa mazao pekee.

 

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi