loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tumtegemee Mungu na si kumtegea

WATANZANIA kama walivyo watu wa mataifa mengine, tupo katika vita dhidi ya maradhi yakiwamo yanayoambukizwa kwa njia ya hewa ukiwamo Uviko (ugonjwa wa virusi vya korona)maarufu, Covid-19.

Tunamshukuru Rais John Magufuli kwa kuwa sambamba na viongozi wa dini kuhimiza Watanzania tumtangulize na kumtegemea Mungu ili tushinde katika mapambano haya ambayo wasiotutakia mema, wanaweza kuyatumia kama mwanya wa kutuletea ‘ukoloni tiba’ na unyonyaji wa kiuchumi tusipokuwa wasikivu kwa wataalamu na viongozi wetu.

Hii ni kusema kuwa, tusikile na kufuata anayoyasema Mkuu wa Nchi kwa kuwa anajua mengi kuliko sisi, tufuate maelekezo ya wataalamu na tumsikilize Rais Magufuli na viongozi wa dini kwa kuomba huruma wa Mungu ili atuepushie janga hili kwani peke yetu, hatuwezi kitu.

Hata hivyo wakati tukimtegemea Mungu, lazima tuhakikishe pia hatumtegei na badala yake, tunapambana huku tukilia kuomba huruma wa Mungu.

Kumtegea Mungu badala ya kumtegemea, ni kupuuza juhudi na maelekezo ya wataalamu na Serikali kuhusu namna ya kujikinga na kuepuka maambukizi kwetu na kwa wenzetu, na kubaki tu kusema, ‘Mungu mwenyewe anajua.” Hilo ni kosa.

Tukiwa wawajibikaji na wakweli, tutakubali ukweli kuwa hakuna hata siku moja ambayo kiongozi yeyote wa dini, serikali au wataalamu wa afya walipoelekeza tuzembee, tulale usingizi na kutegemea miujiza ya kuhamisha milima maan lazima tujisaidie, ili tumwombe Mungu atusaidie.

Ili tusimtegee Mungu, kila mmoja achukue tahadhari zote kisha, amwombe Mungu aziwezeshe juhudi zetui kufanikiwa.

Hizi ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara kwa majitiririka na sabuni, kuepuka misongano isiyo ya lazima na kutumia sawia vizibauso (barokoa) na wakati huo huo, tukimwomba Mungu atuhurumie maana.

Sisi tufanye sehemu yetu, kisha tumwombe na kumtanguliza Mungu tukitegemea ukamilifu wake, vinginevyo kama tutalala, tutakuwa  tunamtegea Mungu, badala ya kumtegemea.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

 

Swali: Nia ya kufunga ...

foto
Mwandishi: Joseph Sabinus

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi