loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Saudia yakanusha tuhuma za Marekani

SERIKALI ya Saudi Arabia imekanusha ripoti ya kijasusi iliyotolewa na Marekani, ikimtuhumu Mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo, Mohammed bin Salman kuwa aliidhinisha mauaji ya mwandishi wa habari wa Gazeti  la Washington Post, Jamal Khashoggi mwaka 2018.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia, imesema serikali inaipinga ripoti hiyo, ikisema imejaa taarifa za uzushi na tathmini isiyokubalika kuhusu utawala wa huo wa Kifalme.

Tathmini ya Marekani kutoka ripoti pana ya kijasusi imedai kuwa Mwana wa Mfalme aliidhinisha operesheni ya kumkamata au kumuua Khashoggi mjini Istanbul nchini Uturuki.

Huko nyuma Saudi Arabia ilishasema kuwa mauaji ya Khashoggi kwenye ubalozi mdogo wa Saudi Arabia, yalifanywa katika operesheni ya kihalifu na kukanusha kuhusika kwa Mtoto wa Mfalme Salman.

"Kwa bahati mbaya kuwa ripoti hii ikiwa na hitimisho lisilo sahihi, imetolewa wakati utawala wa kifalme umekwishakosoa uhalifu huo wa kutisha, na uongozi wa Saudia ulichukua hatua zinazohitajika kuhakikisha kisa kama hicho hakitokei tena," ilisema sehemu ya taarifa ya wizara hiyo ya Wizara ya Mambo ya Nje.

Jamal Khashoggi aliuawa akiwa na miaka 59 akiwa uhamishoni Marekani. Alikuwa akiandika ripoti zinazomkosoa Mohammed bin Salman na serikali ya Saudi Arabia. Aliuawa mwezi Oktoba mwaka 2018.

Mwandishi huyo aliitwa na Balozi wa Saudia mjini Istanbul afike katika ubalozi huo, ili kupata nyaraka kadhaa alizohitaji ili aweze kufunga ndoa na mpenzi wake, raia wa Uturuki, Hatice Cengiz.

KAMATI ya Kuratibu Ushirikiano wa ...

foto
Mwandishi: RIYADH, Saudi Arabia

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi