loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wizara ya Kilimo, JKT wakubaliana kilimo endelevu

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) na Wizara ya Kilimo zimetiliana saini mkataba wa makubaliano wa miaka mitano ili kuhakikisha kunakuwa na kilimo endelevu ili kuchangia uchumi na kuinua pato la taifa.

Maeneo ambayo makubaliano hayo yatafanya kazi ni usambazaji wa teknolojia bora katika uzalishaji mazao ya chakula na biashara, kujenga uwezo wa kusambaza huduma za ughani, huduma za kitaaluma katika miundombinu ya kilimo, utafiti na masoko, huduma za kusimamia mazao baada ya mavuno na uongezaji wa thamani za mazao ya kilimo na kuhamasiha mbinu za uzalishaji na kilimo vumilivu.

Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Charles Mbuge, alisema makubalinano hayo yamelenga kuimarisha kilimo kwa manufaa ya nchi .

“JKT ina jukumu la kuzalisha mali na kulea vijana, hivyo vijana wa kujitolea wanaokaa miaka miwili watapata mbinu bora za kilimo watakazozisambaza nchi nzima,” alisema.

Alisema JKT ina maeneo makubwa na kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara na mkakati wa jeshi hilo katika kipindi cha miaka mitano ni kulima ekari 26,500 za mazao ya chakula na kati ya hizo ekari 12,000 zitalimwa kilimo cha umwagiliaji.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya, alisema makubalinano hayo yatatekelezwa kwa miaka mitano na kufanyiwa mapitio baada ya muda huo kupita.

“Miongoni mwa mambo ambayo watatekeleza kwa pamoja ni kuanzisha utafiti wa pamoja katika sekta ya kilimo, kusambaza zana za kilimo na taarifa za kilimo na masoko,” alisema.

Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa JKT na ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Kanali Hassan Mabena, alisema tangu kuanza kilimo mkakati, JKT imepata mafanikio kadhaa ikiwamo ununuaji wa zana za kisasa za kilimo, ujenzi wa skimu ya umwagiliaji kwa kutumia fedha za ndani na kuongeza uzalishaji.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi