loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Madaktari bingwa kutoka Cuba watua Muhimbili

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea jopo la madaktari bingwa na wauguzi 10 kutoka nchini Cuba waliowasili juzi kushirikiana kutoa tiba, kuwajengea uwezo wataalamu wazalendo nchini na kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru, alisema hayo wakati akiwapokea wataalamu wabobezi katika fani mbalimbali watakaokuwa nchini kwa miaka miwili.

Alisema hospitali hiyo imepokea wataalamu hao kutoka Cuba ikiwa ni awamu ya pili tangu mwaka 2017 ilipoamua kushirikiana na wataalamu wabobezi kutoka Cuba ili kubadilishana uzoefu.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, sababu ya kushirikiana na wataalamu wabobezi kutoka Cuba ni kuitikia mwito wa serikali wa kupunguza rufaa za wagonjwa kutibiwa nje ya nchi na kwamba, hospitali hiyo ilikarabati miundombinu ya kutolea huduma, na kufanya ununuzi wa vifaa tiba na kuwa na wataalamu wa kutoa tiba hizo.

“Baada ya maboresho makubwa tuliyoyafanya, likaja suala la rasilimali watu, hivyo tukaamua kupeleka wataalamu nje ya nchi kujifunza, lakini pia tuliwaleta wataalamu kutoka nje kuja kufanya kazi na sisi na kutoa ujuzi kwa wataalamu wetu,” alisema Maseru.

Akaongeza: “Uamuzi wa kupeleka wataalamu nje, pia ulifanyika wakati wa maandalizi kuanzisha huduma ya kupandikiza vifaa vya kusaidia kusikia na upandikizaji figo na sasa madaktari wazalendo wanafanya upasuaji wa kupandikiza figo wenyewe."

Alisema njia nyingine iliyotumika kuboresha huduma za afya ni hospitali kuingia makubaliano ya kuleta madaktari na wauguzi 16 kutoka  Cuba mwaka 2017 waliofanya kazi kwa miaka miwili. Wataalamu 11 kati yao, wamesharejea Cuba.

“Mwaka 2019 tuliingia mkataba mwingine na nchi ya Cuba na kupatikana kwa wataalamu hawa 10 ambao kwa awamu hii jukumu lao kuu litakuwa kuwafundisha wataalamu wazalendo na watafanya kazi katika hospitali zetu zote za Upanga na Mloganzila," alisema Profesa Museru.

Kiongozi wa Wataalamu kutoka Cuba, Dk Miguel Oconnor, aliahidi kushirikiana na wataalamu wazalendo kutoa huduma mbalimbali kwa wagonjwa wanaofika Muhimbili.

Wataalamu hao walitembelea maeneo mbalimbali ya kutoa huduma, ikiwamo wodi ya watoto wachanga wanaohitaji uangalizi maalumu, vyumba vya upasuaji na wodi ya wagonjwa kwa kina mama wanaohitaji uangalizi maalumu.

Miongoni mwa wataalamu hao, wamo wataalamu wa uuguzi, wataalamu wa usingizi, madaktari wa wodi za wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu na watalaamu wa  upasuaji wa macho.

 

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi