loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Fedha za Tasaf si kwa ulevi, kuoa’

MKUU wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, John Mwaipopo, amewataka wananchi wanaonufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini ulio chini ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), kutotumia kutumia fedha wanazopewa kwa kuolea wanawake au kunywea pombe badala yake, wazitumie kuwekeza katika miradi mbalimbali ya kiuchumi.

Alibainisha hato katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Iborogelo alipokuwa akizungumza na baadhi ya wananchi wanaonufaika na mpango huo kijijini Iborogelo.

Mwaipopo alisema kutumia fedha hizo kuoa wanawake au kwa starehe katika vilabu vya pombe, ni kwenda kinyume na dhamira ya serikali matumizi ya fedha hizo, kwa kuwa fedha za Tasaf si kwa jili ya kuolea au ulevi.

Alisema serikali iliamua kuweka mpango huo ili kuzisaidia kaya masikini kuondokana na umasikini, hivyo kila mnufaika wa Tasaf ana wajibu kuzitumia kwa miradi mbalimbali ya kiuchumi ukiwemo ufugaji wa kuku, mbuzi, na  katika kilimo cha mazao ya biashara bila kusahau kuwpeleka watoto shule na katika huduma za afya kama kliniki.

Aliwapongeza wananufaika wa mpango huo waliotumia fedha wapatazo kuwekeza katika ufugaji, kilimo, na elimu kwa kununulia watoto waomahitaji ya shule na kuwataka waendeleze juhudi zao.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Iborogelo, Juma Mayunga, alisema katika taarifa ya kijiji hicho kuwa, kaya 125 kijijini hapo zinanufaika na mpango huo.

Alisema walengwa wamekuwa wakipata mafunzo ya kuwekeza katika rasilimali zalishi kipindi chao kitakapoisha, wawe wamejiendeleza na kujikwamua kiuchumi.

Diwani wa Kata ya Iborogelo, Emmanuel Busongo, aliwataka wananchi wanaonufaika na mpango huo kutoka Tasaf kuzitumia fedha hizo kama wanavyofundishwa akisema atakuwa mfuatiliaji wa fedha hizo.

Baadhi ya wanufaika wa mpango huo kijijini Iborogelo, Amina Maganga aliyepokea Sh 68,000 na Johari Makala aliyepokea Sh 66,000 kwa nyakati tofauti walisema fedha hizo zimewasaidia kupata maeneo ya kukodi mashamba kwa ajili ya kilimo, kufuga kuku, mbuzi na hadi sasa hali zao ni nzuri.

Mratibu Msaidizi wa Mapango wa Kunusuru Kaya Masikini katika Wilaya ya Igunga, Richard Mtamani, alisema wamehaurisha Sh  274,464,000 katika vijiji 57 vyenye kaya 4766.

Kwa mujibu wa Mtamani, fedha hizo ni za Novemba na Desemba 2020 na kubainisha kuwa, kabla ya zoezi hilo wamekuwa wakitoa elimu kwa walengwa wote na kufanya uhakiki kabla ya kuhaurisha.

 

 

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Tabora

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi