loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bumbuli washangalia kiwanda cha chai kurejesha uzalishaji

WAKAZI wa Bumbuli wilayani Lushoto wameishukuru serikali kwa kurejesha uzalishaji katika kiwanda cha Mponde Tea Estate kilichopo Kata ya Mponde wilayani humo.

Wametoa shukrani hizo wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, alipozuru kiwanda hicho kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majiliwa kuwa, kiwanda hicho kianze kufanya kazi.

Katika ziara hiyo, Waziri Mhagama alisema serikali imeamua kufufua kiwanda hicho ili wakulima wa chai waendelee kulima zao hilo na liwaletee manufaa.

“Serikali imeamua kurejesha matumaini kwa wakazi wa Bumbuli na Wilaya ya Lushoto kwa kuanzisha shughuli za uzalishaji katika Kiwanda cha Mponde Tea Estate ili kuhakikisha kilimo cha chai kinaleta tija na kusaidia wakulima wa zao hilo waliopo katika maeneo hayo kunufaika zaidi,” alisema Mhagama.

Alisema serikali imedhamiria kuanzisha shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho ili kuwezesha wakazi wa Bumbuli na Lushoto kwa jumla, kuongeza uzalishaji wa zao hilo kwa kuwa na soko la hukakika.

Kwa mujibu wa Waziri Mhagama, Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020 – 2025, imeweka chai kuwa moja ya mazao ya kimkakati, hivyo serikali imejipanga kuongeza uzalishaji wa zao hilo kutoka takriban tani 37,000 zinazozalishwa sasa hadi zaidi ya tani 60,000 ifikapo mwaka 2025.

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, January Lugangika, alisema kata 18 zilizopo katika wilaya hiyo zinalima zao la chai na asilimia kubwa ya wakulima wa zao hilo wana matumaini makubwa katika kiwanda hicho kuwainua kiuchumi kutokana na ajira watakazopata kiwandani hapo na kuuza malighafi ya zao la chai.

Naye Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, aliwataka wakazi hao kuchangamkia fursa ya kuzalisha chai kwa wingi kwa kuwa serikali imeamua kuanzisha uzalishaji katika kiwanda hicho.

“Migogoro iliyojitokeza katika kiwanda hiki awali ilichangia kudhorotesha uchumi wa wakazi wa maeneo haya kwa sababu wananchi wengi waliacha kulima chai baada ya kiwanda kufungwa, lakini kuanzishwa shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho kutahamasisha wakulima wengi kulima chai na kunufaika kiuchumi,” alisema Makamba.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo  Juma Msilimu alimshukuru Rais John Magufuli kwa kurejesha matumaini kwa wananchi hususan wakulima wa zao hilo wilayani Lushoto kutokana na uwepo wa kiwanda cha Mponde Tea Estate.

 

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Lushoto

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi