loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

WMA yapata mwarobaini malipo matumizi ya umeme

WAKALA wa Vipimo (WMA) umesimika mtambo wa kisasa wa kupima mita za umeme kuhakikisha wananchi wanalipia kiasi sahihi cha nishati wanayotumia.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa wakala huo, Stela Kahwa wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe.

Naibu Waziri huyo alitembelea kituo cha WMA Misugusugu Kibaham mkoa wa Pwani kuangalia maendeleo ya kituo hicho kinachopima ujazo sahihi wa matangi ya magari ya mafuta, upimaji wa mita za maji na za umeme.

Stela alimweleza Kigahe kuwa kufungwa kwa mtambo huo wa kupima mita za umeme ni utekelezaji wa maagizo ya serikali kwa WMA.

“Tunashukuru kwamba tumeyatekeleza maagizo hayo yote ya serikali kwa wakati, mtambo umefungwa na mita za umeme zinaanza kupimwa ili kuleta tija na thamani iliyokusudiwa na hadi Machi 15 tutaanza kupima mita hizo kwa kasi,” alisema.

Kwa upande wake, Kigahe alielezea kufurahishwa na maendeleo ya kituo hicho na kuwataka watendaji wa WMA kuendelea kukisimamia kwa kutumia weledi.

Alisema kutokana na maboresho yaliyofanyika, hivi sasa magari 70 yanayosafirisha mafuta yanapimwa kwa siku hali inayowarahishia wafanyabiashara kwenda na wakati.

Kuhusu mita za maji, Naibu Waziri huyo alisema serikali imenunua mtambo huo kwa gharama ya Sh milioni 500 na kwamba mita zote za maji hupimwa kabla ya kufungwa.

Alisema hali hiyo imesaidia kuondoa malalamiko ya wananchi ambao wamekuwa wakilalamikia mita ambazo huwapunja maji wanapofungiwa.

“Malalamiko kwamba mita za maji wanazofungiwa ni feki yalikuwa mengi mno, sasa kupitia mtambo huu tunakuwa na uhakika kwamba mita inayokwenda kufungwa kwa mteja na taasisi nyingine zinakuwa sahihi kwa sababu zinasoma vipimo sahihi.”

“Mita nyingi zimekuwa zikilalamikiwa sasa mita zote zipitie hapa zipimwe kwanza ili mteja anapofungiwa ziwe na usahihi na awe analipa kile anachostahili kutokamna na matumizi yake.”

“Tunaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa uwekezaji huu wa zaidi ya Sh bilioni nane na katika awamu nyingine tunataka kwenda kupima gesi,” alisema na kuongeza:

“Baada ya kukamilika awamu hii tutakwenda kupima ujazo wa gesi na tutakapokamilisha waziri anaweza kumwalika Rais atufungulie majengo haya,” alisema

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Riziki Shemdoe alisema mradi wa Misugusugu una sehemu nne ambazo ni ya kupima ujazo wa matangi ya magari ya mafuta,  kupima mita za maji na sehemu ya kupima mita za umeme.

Alisema ujenzi wa majengo mapya kwenye eneo hilo umefanywa bila kutumia mkandarasi na ndiyo sababu gharama zake ziko chini.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Pwani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi