loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Katwila matumaini kibao Ihefu

KOCHA wa Ihefu FC, Zuber Katwila amesema kuimarika kwa kikosi chake tangu kuanza mzunguko wa pili kunampa matumaini ya  kuendelea kusalia kwenye Ligi Kuu msimu ujao.

Ihefu ambayo inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza, inashika nafasi ya 16 kwenye msimamo ikiwa imekusanya pointi 21 katika michezo 21 iliyocheza mpaka sasa. 

Akizungumza na gazeti hili jana, Katwila alisema usajili alioufanya kwenye dirisha dogo umemsaidia kuirudisha timu hiyo kwenye ushindani wa ligi ambayo ipo katika mzunguko wa lala salama.

“Nashukuru kuona kile ambacho nilichokuwa nataka kukiona kwenye timu yangu hivi sasa ndio kinatokea, tumecheza mechi tatu na kushinda mbili na sare moja kwetu ni matokeo mazuri ikizingatiwa na tulivyoanza msimu,” alisema Katwila.

Kocha huyo alisema kutokana na mwanzo mzuri walioanza nao mzunguko wa pili, Ihefu haiwezi kushuka daraja kwani wamejizatiti kuhakikisha mechi zote watakazocheza nyumbani kwao wanashinda ili kujiweka sehemu salama.

Katwila alisema kilichokuwa kikiisumbua timu hiyo kwenye mzunguko wa kwanza ni ugeni wa ligi pamoja na asilimia kubwa ya wachezaji kutokuwa na uzoefu lakini wachezaji aliowaongeza kwenye dirisha dogo wenye uzoefu ukichanganya na waliopo wameanza kumpa kile alichokuwa akikihitaji.

Alisema pamoja na kupata matokeo mazuri katika mechi za ligi lakini lengo lao kubwa msimu huu ni kumaliza ligi  ndani ya 10 bora na kama watafanikiwa hilo msimu ujao ndio wataanza kufukiria ubingwa.

Katwila kocha na mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, alijiunga na timu hiyo mwishoni mwa mzunguko wa kwanza akitokea Mtibwa Sugar ambako alibwaga manyanga kufuatia matokeo mabaya yaliyokuwa yakiiandama timu hiyo.

KLABU ya soka ya Simba imeingia mkataba ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi