RAIS wa zamani wa Marekani, Donald Trump amesema hana mpango wa kuanzisha chama kipya cha siasa na badala yake ameahidi kuwa ataendelea kuungana na wana Republican.
Ameeleza hayo jana katika hotuba yake kupitia mkutano wa ‘Conservative Political Action Conference’ (CPAC).
Hiyo ni hotuba yake kubwa ya kwanza tangu aondoke madarakani mwezi uliopita, Januari 20, 2021 baada ya wadhifa wake kuchukuliwa na Rais wa sasa, Joe Biden.
Aidha, alisema kuwa Chama cha Republican kitaungana na kuwa na nguvu zaidi ya ile iliyokuwepo hapo awali.