loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pepe amuumbua Beki wa zamani wa Arsenal

Beki wa zamani wa Arsenal, Tony Adams amesema winga wa timu hiyo, Nicolas Pepe amemthibitishia kuwa mtazamo wake juu yake, katika mechi dhidi ya Leicester City, haukuwa sahihi.


Alisema hayo jana baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa King Power, ambapo Arsenal ilijizolea alama tatu za ugenini kwa kuichalaza Leicester mabao 3-1, katika mchezo wa Ligi Kuu.


Amesema katika mechi hiyo, Pepe alikuwa kwenye kiwango bora tofauti na matarajio yake, na kuongeza kuwa  mchezo wake wa jana ni moja ya michezo bora katika msimu huu.


Winga huyo wa kimataifa kutoka Ivory Coast, aliipatia Arsenal bao la tatu na la mwisho katika mchezo huo, dakika ya 52. 


Mabao mengine katika mchezo huo yalifungwa na David Luiz (39’) na Alexandre Lacazette (45+2’) kwa mkwaju wa penati, huku bao pese la Leicester likifungwa na Youri Tielemans (6’).

KLABU ya soka ya Simba imeingia mkataba ...

foto
Mwandishi: LONDON,England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi