loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TFF yafafanua kuhusu mechi ya Simba FA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ufafanuzi juu ya mchezo wa ‘Azam Sports Federation Cup’ (ASFC), hatua ya 16 bora kati ya timu ya Simba na Kagera Sugar ambao ulipangwa kuchezwa Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.


Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Ofisa wa Habari na Mawasiliano wa shirikisho hilo, Cliford Ndimbo amesema kuwa ratiba ambayo ilitolewa na TFF iko sahihi kwa mujibu wa droo iliyochezeshwa Februari 09.


Aidha, taarifa hiyo imesema ratiba ambayo inasambaa mtandaoni inayoonesha Kagera Sugar inastahili kuwa nyumbani katika mchezo huo, ni ratiba ambayo ilikuwa na makosa ya kiuandishi kwa AzamTV ambao pia walifanya marekebisho baada ya kugundua makosa hayo.


Pia imeeleza kuwa ratiba hiyo haikuwahi kubadilishwa kwa namna yoyote ile na ni vyema timu zikazingatia na kufuatilia wakati droo inapofanyika.

KLABU ya soka ya Simba imeingia mkataba ...

foto
Mwandishi: Isdory Kitunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi