loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dk Mwinyi:Waandishi fanyeni uchambuzi

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amewataka waandishi wa habari, wabadilike na kufanya uchambuzi wa matukio kitaalamu zaidi, badala ya kutoa taarifa kwa kuwa kazi hiyo siku hizi inafanywa na mitandao ya kijamii.

Alisema wananchi wanastahili kufahamu kazi zinazofanywa na serikali zao na malengo ya kukuza uchumi na maendeleo kuliko kutoa taarifa za matukio ya kila siku.

Dk Mwinyi aliyasema hayo Kikwajuni Unguja wakati akifungua Kongamano la Kujadili Matumizi ya Sekta ya Mawasiliano ya Habari kuijenga Zanzibar mpya.

Alisema katika siku 100 tangu aingie madarakani, amebaini kwamba hakuna mfumo mzuri wa kupokea taarifa za wananchi.

''Ndiyo maana nimeanzisha mfumo wa kuwasiliana na Rais ''Sema na Rais'' kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata taarifa zao moja kwa moja na kuratibiwa na ofisi yangu''alisema Dk Mwinyi.

Alisema uandishi wa habari ni kazi ya taaluma, kwa hivyo haiwezi kufanywa na kila mtu bila ya kusomea.

“Wakati umefika kwa waandishi wa habari kusomea taaluma hiyo...kazi ya uandishi wa habari haiwezi kufanywa na kila mtu bila ya kusomea...tunataka uandishi wa habari wa kufanya uchambuzi wa matukio kitaalamu zaidi na kuwafikia wananchi''alisema Dk Mwinyi.

Aliwataka waandishi wa habari, watumie vizuri kalamu zao, kuiwezesha Serikali ya Awamu ya Nane kudumisha maridhiano ya kisiasa ili kuondoa siasa za chuki na uhasama.

Alivitaka vyombo vya habari, vihubiri amani na utulivu kwa kuwa maridhiano yaliyofikiwa, yanatoa nafasi kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kutekeleza malengo ya kufikia uchumi wa bluu.

Alisema katika siku 100 amefanya kazi ya kujenga uwajibikaji serikalini, hivyo kurudisha nidhamu ya watumishi wa serikali kwa kiasi kikubwa.

“Katika kipindi cha siku mia moja tumefanya mambo mengi ikiwemo uwajibikaji wa watendaji wetu pamoja na vita dhidi ya rushwa na uhujumu wa uchumi...haya yote nawaomba waandishi wa habari wayafanyiye kazi vizuri”alisema Dk Mwinyi.

Mapema Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Mwita Maulid aliwataka maofisa habari wa wizara, watoe taarifa kwa waandishi wa habari ili wananchi wafahamu kazi nzuri zinazofanywa na SMZ.

“Moja ya changamoto kubwa ya waandishi wa habari ni kukosa taarifa kutoka kwa watendaji wa Serikali, hatua ambayo ni kikwazo na kuwafanya wananchi kushindwa kujua Serikali yao inachokifanya...maofisa habari kazi yenu ni kutoa habari na sio kuficha taarifa za serikali”alisema.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi