loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Sina haraka na Bocco- Gomes

KOCHA Mkuu wa miamba ya soka Tanzania, Didier Gomes amesema licha ya nahodha wake, John Bocco kupona majeraha yaliyomweka nje kwa muda mrefu, hatakuwa na haraka ya kutaka kumtumia ili kumsaidia kupona vizuri.

Bocco tayari ameanza kufanya mazoezi na wenzake na alicheza kwa dakika chake mchezo uliopita wa Kombe la FA dhidi ya African Lyon ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 na kusonga mbele hatua ya 16 bora.

Akizungumza na gazeti hili jana, Gomes alisema anatambua mchango wa Bocco kwenye kikosi cha Simba lakini kumpa muda mrefu wa kucheza ni hatari kwa afya yake na klabu sababu wapo kwenye michuano migumu inayohitaji kila mchezaji kuwa sawa.

“Natambua uwezo alionao Bocco, ni mshambuliaji hatari lakini ametoka kwenye kuuguza majeraha ingawa ameanza mazoezi na wenzake lakini anapaswa kupata muda mchache wa kucheza ili asije jitonesha lakini pia aweze kuendana na kasi waliyonayo wenzake,” alisema Gomes.

Kocha huyo alisema haoni haja ya kumharakisha kupona mchezaji huyo sababu kuna washambuliaji watatu hadi wanne kwenye kikosi chake hivyo pamoja na kutambua umuhimu wake atamvumilia mpaka atakapojiridhisha kuwa yupo tayari kumpa majukumu makubwa.

Alisema yeye na jopo la madaktari wa Simba watamfuatilia na kumsaidia mchezaji wao ili kuhakikisha anarejea kwenye kiwango chake na kuipigania timu hiyo katika harakati zake za kufanya vizuri kwenye mashindano yote inayoshiriki.

Bocco anayeshika nafasi ya pili kwa ufungaji kwenye timu hiyo na Ligi Kuu kwa ujumla akifunga mabao manane, alipata majeraha ya goti kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 na kufuzu hatua ya makundi.

KLABU ya soka ya Simba imeingia mkataba ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi