loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kocha wa Rwanda aongezewa mkataba

KOCHA wa timu ya taifa ya Rwanda, Amavubi, Vincent Mashami amesaini mkataba wa mwaka mmoja baada ya kufika robo fainali za michuano ya mabingwa wa Afrika, Chan 2020, Januari mwaka huu. 

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 38 ana kibarua kigumu cha kuiongoza timu hiyo kwenye michuano ya kufuzu Afcon 2021 na Kombe la Dunia Qatar 2022. 

Mashami amekuwa kocha wa timu ya taifa ya Rwanda tangu Agosti 2018 na mkataba wake ulimalizika  Februari 11.

Rwanda itaikaribisha Msumbiji kwenye mechi ya kufuzu Afcon 2021 Machi 22 kabla ya kucheza na Cameroon Machi 30. 

Rwanda iko mkiani mwa kundi F ikiwa na pointi mbili, Cameroon inaongoza kundi ikiwa na pointi 10, huku Cap-Verde na Msumbiji zikiwa na pointi nne kila moja. 

Wakati huohuo, Amavubi itaanza kampeni za kufuzu Kombe la Dunia Juni na imepangwa Kundi E pamoja na Mali, Uganda na Kenya.

KUMEKUWA na zogo kwenye soka la Ulaya tangu ...

foto
Mwandishi: KIGALI, Rwanda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi