loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Klopp: Tupo sehemu ya kufurahisha

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kikosi chake bado kipo sehemu ya kufurahisha baada ya kuifunga Sheffield United ikitoka kufungwa mechi nne mfululizo.

Katika mechi hiyo, mlinda mlango wa Blades, Aaron Ramsdale alipanga safu yake na kuokoa michomo mingi ya Liverpool katika kipindi cha kwanza.

 

Lakini Curtis Jones mwenye umri wa miaka 20 alionesha kuguswa na wachezaji wenzake walivyokosa na kuvunja ngome ya wenyeji muda mfupi baada ya kutoka mapumziko.

 

Jaribio la Roberto Firmino lilimfanya Kean Bryan kujifunga na kuifanya Liverpool kuwa na jumla ya mabao 7,000 hadi sasa.

 

Reds ni timu ya pili kufikia alama hiyo baada ya wapinzani wao wa Merseyside Everton ambao wamefunga mabao 7,108.

 

"Watu wengi wametuandikia. hiyo ni sawa," alisema Klopp ambaye timu yake inashika nafasi ya sita ikiwa nyuma kwa pointi mbili nyuma ya West Ham inayoshika nafasi ya nne. 

 

"Pamoja na shida zote ambazo tumekuwa nazo bado tuko karibu na maeneo ya kufurahisha.”

 

"Hii ilikuwa juu ya sisi kuonesha bado tupo. Tutacheza na Chelsea Alhamisi lazima tuionyeshe tena, lazima tushinde michezo, tunajua hilo. Hakuna njia ya kuingia kwenye ligi ya mabingwa bila matokeo."

 

Sheffield United walionesha ushindani muda wote wa mchezo na Oliver McBurnie angefanya vizuri kama siyo kichwa cha krosi ya Oliver Norwood kwenda nje.

Lakini Blades wanaoshika nafasi ya chini wanalazimika kutengeneza ahueni ili wabaki kwenye Ligi Kuu msimu huu.

Ni miezi nane tu tangu Liverpool ilipotwaa taji lao la kwanza la ligi kwa miaka 30 lakini kikosi cha Klopp kililazimika kubadilisha matarajio yao msimu huu na sasa wanajikuta katika vita ya kufanikiwa kushika nafasi nne bora kupata kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.

KUMEKUWA na zogo kwenye soka la Ulaya tangu ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi