loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais wa Barcelona  akamatwa na polisi

RAIS wa zamani wa Barcelona, Jose Maria Bartomeu anashikiliwa na polisi baada ya kuhusishwa na tuhuma ya kurubuni kampuni mbalimbali za mitandao ya kijamii kuandaa kampeni maalumu ya kuwashambulia watu na taasisi zilizokuwa zinapinga utawala wake.

Bartomeu ambaye alihudumu kwenye klabu hiyo kwa miaka kadhaa, alijiuzulu Oktoba, mwaka jana, alikamatwa baada ya maofisa wa usalama kutembelea ofisi za klabu hiyo kwa ajili ya kusaka nyaraka muhimu zitakazo husika kwenye tuhuma hizo.

Vyombo vya habari vya Hispania vilisema operesheni hiyo inahusiana na ‘Barça-gate’ ya mwaka jana, ambapo maofisa wa klabu hiyo walituhumiwa kuanzisha kampeni ya ‘smear’ dhidi ya wachezaji wa sasa na wa zamani ambao walikuwa wakikosoa klabu na Bartomeu anashikiliwa kwa madai ya kuajiri kampuni za mitandao ya kijamii kuwadharau hadharani.

 

Baadhi ya kampuni zilizotajwa kuhusika kwenye tuhuma hizo ni NSG Social Science Ventures SL, Tantra Soft SA, Digital Side SA, Big Data Solutions SA na Futuric SA na hii ni kwa mujibu wa jarida la michezo la kuaminika nchini Hispania la Marca.

Licha ya kushikiliwa na polisi, lakini Bartomeu alikana kuhusika kwenye tuhuma hizo.

Yeye, mtendaji mkuu wa sasa Oscar Grau na mkuu wa huduma za sheria wa Barcelona, ​​Román Gómez Pontí walikamatwa kwa tuhuma za utawala mbovu, ufisadi na utapeli wa fedha, kwa mujibu wa kituo cha radio cha Cadena SER.

Polisi wamethibitisha kuwa wamewakamata watu kadhaa, bila kuthibitisha idadi au utambulisho wa waliowekwa kizuizini.

Bartomeu na bodi yake ya wakurugenzi walijiuzulu mwaka jana wakati wa mzozo wa Lionel Messi. 

Klabu hiyo imejaa machafuko ya kisiasa na deni likisababishwa na janga la corona.

Operesheni hiyo inakuja chini ya wiki moja kabla ya uchaguzi wa rais kufanyika na zaidi ya wanachama wa Barcelona 20,000 tayari wamepiga kura kupitia posta.

Wagombea watatu, Victor Font, Joan Laporta na Toni Freia wako kwenye kura ya mwisho muhimu ya kumpata rais.

Hii ni mara ya pili polisi kutembelea ofisi za klabu ya Barcelona na kufanya ukaguzi kuhusiana na kesi hiyo, kwani mwishoni mwa mwaka jana Jaji wa mahakama inayosimamia kesi hiyo aliamuru klabu ikaguliwe na jana wamekagua kwa mara ya pili.

KUMEKUWA na zogo kwenye soka la Ulaya tangu ...

foto
Mwandishi: BARCELONA, Hispania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi