loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Gharama za kupiga simu zashuka 

MAMLAKA ya Mawasiliano (TCRA), imesema gharama za kupiga simu pasipo kujiunga kifurushi zimeshuka kutoka Sh 290.27 hadi  70.81 kwa dakika.

Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema kuwa kwa kulinganisha mwaka 2018 na Februari 2021, wastani wa bei za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mtandao mwingine pasipo kujiunga na kifurushi nazo zimeshuka kutoka Shillingi 387.55 hadi 71.99 kwa dakika, sawa na punguzo la 81%.

Amesema bei za kutuma jumbe fupi (SMS) zimeshuka kutoka Shillingi 64.12 hadi 22.23 kwa ujumbe mmoja sawa na punguzo la 65%.

Aidha wastani wa bei za data kwa 'MB' moja pasipo kujiunga na kifurushi zimeshuka kutoka Shillingi 104.86  mpaka 24.16.

Kilaba amesema lengo kubwa ni kupunguza tofauti kubwa iliyokuwepo kati ya bei za vifurushi na bei za kutumia huduma bila kujiunga na vifurushi.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi