loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TCRA: Toeni taarifa matumizi ya vifurushi

MAMLAKA ya Mawasiliano (TCRA), imezitaka kampuni za simu kutoa taarifa kila wakati za matumizi ya vifurushi yatakapofikia  75% na 100%  kwa vifurushi vya muda wa maongezi, data na ujumbe fupi (SMS)

Mkurugenzi wa TCRA, James Kilaba amesema  mtoa huduma ataweka Program Rununu (Mobile App) ya kumwezesha
mtumiaji wa huduma mwenye simu janja kufuatilia matumizi yake ya data kwa kupakua Program Rununu hiyo ya mtoa huduma.

“Tumewataka waweke  utaratibu unaowawezesha anayejiunga na huduma za vifurushi kuchagua na kukubali kutozwa gharama zisizokuwa kwenye vifurushi mara muda wa vifurushi alichojiunga nacho au uniti za kifurushi husika kumalizika." alisema Kilaba

Alisema utaratibu huu wa kuchagua na kukubali utakuwa chaguo la msingi mpaka pale anayejiunga achague na kukubali kutumia gharama nje ya kifurushi.

Alisema pia mtoa huduma ataweka utaratibu wa kumwezesha aliyejiunga na kifurushi chochote kuendelea kutumia muda au uniti za kifurushi ambazo zitakuwa zimesalia ndani ya muda wa matumizi uliowekwa kwa kununua tena kifurushi hicho hicho kabla ya kumalizika kwa muda wake.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi