Tamasha la kumwombea Samia, Tanzania kutua Arusha

TAMASHA la kuiombea nchi na kumwombea Rais Samia Suluhu Hassan linatarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu jijini Arusha ambapo wasanii mbalimbali wa muziki wa injili wanatarajia kutumbuiza.

Hatua hivyo inatakoana na kuwapo kwa mafaikio ya tamasha la kuliombea nchi lililofanyika jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa HabariLeo Ijumaa Novemba 11,2022, jijini hapa, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama amesema maandalizi kwa ajili ya tamasha hilo yanaendelea vizuri.

Amesema lengo la tamasha hilo ni kuiombea Nchi pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan Mwenyezimungu ampe afya njema pamoja na kumlinda na mabalaa yote.

“Rais wetu Maana ana majukumu mengi kama mnavyoona anasafiri anakwenda kila kona, hivyo ni lazima Rais wetu tumpende tumweke mikomoni mwa Mungu amlinde ili aweze kutuongoza vyema, tuendeleaa kuwa na amani kama mnavyoona nchi yetu.”

Amesema baada ya tamasha la Arusha litafuatiwa na tamasha litakalofanyika Dodoma Desemba 11 mwaka huu na baadae wataelekea Singida na Kahama.

Msama amewataja wasanii watakaoshiriki katika tamasha hilo kuwa ni Rose Muhando, Joshua Mlelwa, Boniface Mwaitege na waimbaji kutoka mataifa mbalimbali huku akidai kiingilio ni bure.

“Niwajulishe wakazi wa Mkoa wa Arusha wakae tayari hakutakuwa na kiingilio litakuwa tamasha kubwa kwa lengo la kwenda mbele za Mungu na kuliombea Taifa na Rais wetu.”

Kwa upande wake Mratibu wa tamasha hilo, Emmanuel Mabisa amesema katika tamasha hilo Kwaya mbalimbali zitatumbuiza na Maaskofu na manabii wa makanisa mbalimbali wanakuepo katika kuwaongoza wananchi kufanya maombi kwa taifa.

“Watumishi wa Mungu wamejipanga maombi yanaendelea tunamuombea Rais kwa sababu ya kazi kubwa anazofanya. Tutaendelea kufanya hivi mpaka hali itakapokuwa shwari wakazi wa Arusha waendelee kujiandaa kama Mwanza.”

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button