loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Profesa Mgaya: Msikimbilie Chanjo, hazina ubora

Mkurugenzi  Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Dawa (NIMR), Profesa Yunus Mgaya amesema Tanzania haina haya ya kukimbilia chanjo na badala yake kuwataka kuwa na subira kwa kuwa ili utafiti wa chanjo ukamilike lazima upitie hatua nne ambazo zinaweza kuchukua hata miaka  10
 Profesa Mgaya alisema chanjo zinazopigiwa upatu hazina ubora wa kitaalamu kuweza kutumiwa na wanadamu kwa sababu ili chanjo ifikie hatua ya kutumiwa na wanadamu lazima ipitie katika hatua kuu  nne.

Hatua ya kwanza baada ya chanjo kutengenezwa inapitia katika hatua ya majaribio ambapo inajaribiwa kwa wanyama kama panya, sokwe na sio binadamu. Baada ya majaribio kwenda vizuri chanjo inapitia hatua ya pili kwa kupata kibali cha kutangazwa katika majarida ya kisayansi.

Profesa Mgaya alisema hatua ya tatu ni ya kujaribisha kwa binadamu wachache kutoka katika mataifa mbalimbali duniani ambapo zoezi hilo litachukua miaka zaidi ya mitatu.

Alisema ikiwa chanjo itafanya vizuri, hatua ya nne ni kujaribiwa kwa watu wengi zoezi linaloweza kuchukua miaka minne na mambo yakiwa mazuri chanjo itasambazwa katika masoko kwa ajili ya biashara katika mataifa mbalimbali.

“Cha ajabu chanjo hii haikuvuka hata hatua ya pili ikapelekwa sokoni hali inayoleta hofu kubwa kwa watumiaji, ndio maana Tanzania tumeamua kuwa na utaratibu wetu wa kushughulikia Corona tupige nyungu sana, tule tangawizi na malimao, tuko salama,” alisisitiza Profesa Mgaya.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi