loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba yaichongea Al Merreihk kwa CAF

UONGOZI wa klabu ya Simba imewasilisha barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na kulitaka  kufanya uchunguzi kuhusu Klabu ya Al Merreikh kuchezesha wachezaji wawili kwenye mchezo dhidi yao, ambao wamefungiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Sudan.

Al Merreikh walicheza na Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika nchini Sudan siku ya Jumamosi Machi 6, 2021na kutoka suluhu.

Wachezaji ambao klabu ya Simba wanataka wafanyiwe uchunguzi ni Ramadan Ajab na Bakhiet Khamis ambao wanadai kufungiwa miezi sita kutokana na kila mmoja kusaini mikataba na timu mbili.

Taarifa kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Barbara Gonzalez inasema adhabu za wachezaji hao zilianza kuanzia Januari 21, 2021.

Simba na Al Merreikh wapo kwenye Kundi A ya Ligi Mabingwa Afrika ambapo mpaka sasa Simba ndiyo kinara wa kundi hilo akiwa na pointi saba, akifuatiwa na AS Vita wenye pointi nne, huku nafasi ya tatu ikishikwa na mabingwa watetezi Al Ahly wakiwa na pointi na Al Merreikh wakishika mkia.

Iwapo CAF wakijiridhisha na madai ya Simba Al Merreikh itaondolewa kwenye michuano hiyo kama Kanuni ya saba ya mashindano ya CAF inavyoeleza na Simba kupewa pointi tatu.

KLABU ya soka ya Simba imeingia mkataba ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi