loader
Dstv Habarileo  Mobile
Tulikosa ubunifu - Gomes

Tulikosa ubunifu - Gomes

KOCHA Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema  ukweli hakufurahishwa na matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons juzi na amegundua walikosa ubunifu wa kutumia nafasi mbalimbali za kufunga.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa Simba ilishindwa kulipa kisasi kwa maafande hao baada ya kulazimishwa sare. Mchezo wa mzunguko wa kwanza wekundu hao walifungwa bao 1-0 ugenini Nelson Mandela, Rukwa.

Akizungumza baada ya mchezo huo Gomes alisema ilikuwa rahisi kwao  kufunga ila kuna baadhi ya mambo hakuweka sawa.

“Tulikosa  ubunifu wa kupiga penalti, upigaji wa faulo na nafasi mbalimbali tulizotengeneza. Haimaanishi kwamba safu yangu ya ulinzi haikuwa vizuri hapana, bado tuko bora ila kwa kweli sikufurahishwa na matokeo,”alisema.

Gomes alisema  sare sio nzuri kwao walihitaji kuendeleza hali ya ushindi kuelekea katika michezo yao ya kimataifa.

Alisema kilichotokea hawezi kuwalaumu wachezaji wake isipokuwa wote wanawajibika kwa kuwa ni sehemu ya timu.

Kocha huyo aliahidi kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika kikosi chake ili kufanya vizuri zaidi michezo ijayo na hasa mchezo ulioko mbele yao dhidi ya Al Merrikh utakaochezwa wiki ijayo.

Kwa upande wa Kocha msaidizi wa Tanzania Prisons Shaban Kazumba alisema siri ya kuwasumbua Simba kwa miaka miwili mfululizo ni kwasababu huwasoma mapema na kujipanga.

Kazumba alisema aliwapa tahadhari wachezaji wake kuwa wasicheze ovyo kwasababu Simba inacheza mpira mfupi mfupi, wakiteleza wanafungwa kwa hiyo wakawa makini kwa maelekezo.

Alisema licha ya kutoka nao sare hawezi kuwadharau aliwaheshimu akijua ni timu nzuri ila anashukuru kwa kuwa mipango waliyokuja nayo ilifanikiwa ingawa walihitaji ushindi na sio sare.

“Sare kwangu haikuwa nzuri,  dakika zilizoongezwa zilikuwa nyingi lakini siwezi kulaumu waamuzi dakika 90 zimemalizika kwa sare, Simba ni timu nzuri ila wamekutana na sisi tunawajua,”alisema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/68ba708a78b00d5e2b8158bb211809e7.jpg

MGOGORO kati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi