loader
Dstv Habarileo  Mobile
Yanga yamrejesha kocha wa viungo

Yanga yamrejesha kocha wa viungo

UONGOZI  wa klabu ya soka ya Yanga, umemrudisha kundini kocha wake wa viungo Edem Mortotsi, kufuatia kubainika kwamba hakuwa akihusiana na matokeo mabaya yaliyokuwa yakiiandama timu hiyo hadi kulivunja benchi la ufundi.

Rai huyo wa Ghana kabla ya kurudishwa kundini alikuwa amehudumu mwezi mmoja klabuni hapo kabla ya uongozi wa Yanga kutangaza kulivunja benchi hilo la ufundi chini ya kocha mkuu  Cedric Kaze raia wa Burundi.

Akizungumza na gazeti hili jana Ofisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli alisema kocha huyo ataendelea kuwa muajiriwa wa Yanga akisaidiana na Juma Mwambusi ambaye amerudishwa nafasi ya kocha msaidizi  wakati huu uongozi ukipambana kutafuta kocha mkuu.

“Uongozi umekaa na kuamua kumrudisha kocha wa viungo Mortotsi, sababu hawakuona kosa lolote kwenye idara yake hivyo kwa sasa ataendelea na ajira yake akisaidiana na Mwambusi tukiamini ataendeleza yale ambayo tulikuwa tunayatarajia kutoka kwake,” alisema Bumbuli.

Msemaji huyo alisema mchakakato wa kumpata kocha mpya atakayeinoa timu hiyo unaendelea vizuri na mpaka kufikia mwishoni mwa wiki ijayo kila kitu kitakuwa kimekamilika.

Alisema wamepokea CV za makocha wengi kutoka mataifa mbalimbali na wanachokifanya hivi sasa ni kuzipitia kwa makini ili kupata kocha bora atakaye ipa timu yao mafanikio katika mbio za Ligi Kuu zinazoendelea hivi sasa.

Hivi karibuni uongozi wa Yanga, ulivunja benchi la ufundi kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambapo timu hiyo imeshinda mechi moja kati ya sita ilizocheza.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/cabf724d1babc121263058d2ede2c4d7.jpg

MGOGORO kati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi