loader
Wanawake wajifua Kombe la Dunia, Afcon

Wanawake wajifua Kombe la Dunia, Afcon

KOCHA wa timu za Taifa za wanawake, Bakari Shime amesema wachezaji wote wapo kambini na wanaendelea na mazoezi yanayofanyika kila siku kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili, Shime alisema wachezaji wote waliingia kambini tangu juzi na wanaendelea na mazoezi ya kujiandaa na michezo ya kufuzu Kombe la Dunia na kufuzu Mataifa ya Afrika (Afcon).

“Nashukuru wachezaji wote wako kambini na wana afya njema na kila siku tunafanya mazoezi viwanja vya Jakaya Kikwete,” alisema Shime.

Shime alisema watakaa kambini kwa wiki mbili kwa sababu wengi wana mazoezi kutokana na kuwa kwenye Ligi Kuu ya Wanawake inayoendelea.

“Kikosi  kitakuwa kambini hadi 22 baada ya hapo watarudi kwenye timu zao kuendelea na Ligi Kuu,” alisema Shime.

Waliopo kambini ni kutoka JKT Queens ni Najat Abbas,  Stumai Abdallah, Donisia Minja, Fumukazi Ally na Mwamvua Seif.

Wanaotoka Simba ni Janeth Shija, Zubeda Mgunda, Julietha Singano, Oppa Clement, Mwanahamis Omar, Fatuma Issa, Vaileth Nicholaus, Kadosho Shekigenda, Koku Kipanga na Dotto Tossy.

Wanaotoka Yanga Princess ni pamoja na  Happy Hezron, Anastanzia Katunzi, Amina Ally, Emiliana Mdimu, Irene Kisisa, Aisha Masaka, Husna Mtunda, Noela Luhala, Neema Charles na Clara Luvanga.

Kutoka Ruvuma Queens kuna Diana Lucas, Ester Mabanza, Enekia Kasonga, Protasia Mbunda, Eva Wailes, Cresta John na Djohari Hamis na Mlandizi Queens kuna Janeth Christopher, Flora Novatus, Shehati Mohamed, Rehema Mohamed na Zainab Ally.

Tanzanite ni Joyce Lema, Neema Majimoto, Sabituna Salim na Hasnat Linus. Wengine ni Diana William na Jamila Mnunduma kutoka Baobab Queens, Hadija Petro (TSC Queens), Aisha Juma kutoka Alliance Girls na Zawadi Hamis kutoka Amani.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e0c783695025f90a58e6a6d408830c00.jpg

WAZRI Mkuu Kassim Majaliwa, amezipongeza klabu za ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi