loader
JPM mzima wa afya

JPM mzima wa afya

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kushikamana, kudumisha amani na wapuuze kauli za chuki zinazotolewa na watu wasioitakia mema nchi kuhusu afya ya Rais John Magufuli kwani ni mzima wa afya.

“Tuendelee kufanya ibada na kupata mawaidha yanayohamasisha amani na utulivu. Rais Dk Magufuli ni mzima wa afya anaendelea na majukumu yake wakati sisi wasaidizi wake tukizunguka kuwahudumia wananchi. Leo (jana) nimezungumza naye na anawasalimia,” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu Majaliwa alitoa kauli hiyo jana baada ya kushiriki swala ya Ijumaa mjini Njombe, ambako alisisitiza kuwa Rais anafanya kazi kulingana na mpango kazi wake.

Alisema wananchi wanatakiwa kushikamana na kuifanya nchi kuendelea kuwa na amani na utulivu.

Alisisitiza wananchi kuendelea kuombea taifa na kuwapuuza baadhi ya Watanzania ambao hawapo nchini na wamekuwa wakitoa kauli za chuki kwa sababu hawapendi maendeleo ya nchi na wanatamani kuona taifa likiporomoka.

“Tuwapuuze baadhi ya Watanzania ambao wamejawa na chuki tu, wamejawa na husda tu na wanatamani kuwachonganisha na kutaka kushuhudia taifa hili likiporomoka,” alisema Majaliwa.

Aliongeza, “Kuanzia juzi hata leo (jana) asubuhi nimeona Watanzania wenzetu wenye husda tena hawako ndani wako huko wanashawishi vyombo vya kimataifa viseme Rais wa Tanzania anaumwa kajifungia hizo ni chuki tu, husda tu.”

“Watanzania tulieni uongozi wenu upo imara na mafanikio tunayaona, kumzushia rais ugonjwa ni chuki, wanasema atoke aende wapi? Ulishamkuta siku moja anazurura Kariakoo? Rais ana mpango wake wa kazi si mtu wa kuzurura,” alieleza Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu alisema Rais Magufuli ana wasaidizi wake kuanzia ngazi ya taifa hadi kijijini na kwamba anafanya kazi kulingana na mpangokazi wake.

Aliwataka Watanzania kuendelea kuwa na amani huku wakiamini serikali yao.

Baadhi ya Watanzania wakiwamo wanasiasa wa upinzani akiwamo aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Tundu Lissu na baadhi ya vyombo vya habari vya nje, wiki hii wametoa taarifa zilizodaiwa kuwa Rais Magufuli ni mgonjwa na alikuwa akitibiwa katika hospitali moja nchi jirani.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2890a8e4ac9fb4d371161fd08a49187f.jpg

RAIS Samia Suluhu Hassan amehutubia taifa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Njombe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi