loader
Dstv Habarileo  Mobile
Simba, Al Merreikh vita ya kimya kimya

Simba, Al Merreikh vita ya kimya kimya

NI vita ya kimya kimya; ndivyo unavyoweza kusema baada ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (Caf) kuzuia mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Simba na Al Merreikh ya Sudan kuchezwa bila mashabiki katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Jumanne ijayo.

Juzi Caf ilitoa taarifa kuwa michezo yote ya Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa itachezwa bila mashabiki.

Baada ya kauli hiyo uongozi wa Simba umejitokeza mbele ya waandishi wa habari na kuwaomba radhi mashabiki kwa sababu ni maamuzi ya CAF ambao ndio wenye mamlaka ya soka Afrika na kusema Simba imezoea kucheza bila mashabiki ikiwa nje ya nchi lakini hapa nchini haijawahi kucheza bila mashabiki.

Akizungumza jana Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara alisema anajua namna ilivyo ngumu kucheza bila mashabiki ila hawana namna lazima waridhie.

 “Tunawaomba mashabiki wetu wasijisikie unyonge, tunajua wapo waliojiandaa kutoka mikoani kuja kutazama mechi ijayo lakini ni maelekezo ya Caf,” alisema.

Alisema kutocheza bila mashabiki walicheza ugenini katika michezo iliyopita na walipata matokeo hivyo wanaamini hata nyumbani ambako walizoea mashabiki watapambana.

Manara alisema wakati klabu hiyo ikitimiza miaka 85 hakumbuki kama waliwahi kucheza bila mashabiki nyumbani hivyo, baada ya mchezo ujao watafuatilia Caf kuona namna ya kurejeshewa mashabiki.

Pia alisema katika mchezo huo watakwenda kuua kimya kimya na wanao uwezo wa kumkata adui yao na kushinda.

“Itakuwa ni vita ya kimya kimya kama ambavyo Simba anawinda. Wachezaji wetu wamezoea kucheza mbele ya mashabiki na wamezoea kucheza bila mashabiki, naamini wana uzoefu wa kutosha kucheza kwenye hali kama hiyo,” alisema.

Aidha alisema wamejipanga kupata pointi tatu ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu kwani watakuwa wanahitaji pointi moja tu kwenye michezo miwili itakayobaki dhidi ya Al Ahly na AS Vita.

Alisema dhamira yao ni kufika nusu fainali ili ile kauli ya Rais John Magufuli aliyotoa mwaka 2018 wachukue ubingwa wa Afrika itimie.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8bd81c9a341424100545f5c9bf767f5b.jpg

MGOGORO kati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi