loader
Dstv Habarileo  Mobile
Stars kujipima kwa Kenya

Stars kujipima kwa Kenya

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo inatarajia kucheza mchezo wa kirafi ki wa kimataifa na timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambe Stars’ katika Uwanja wa Taifa wa Nyayo, Narobi.

Akizungumza na gazeti hili jana kocha mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen alisema wapo tayari kwa mchezo huo na jana walifanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Taifa wa Nyayo utakaonza saa 9:00 alasiri.

“Wachezaji wote wako salama na leo (jana) wamefanya mazoezi kujiandaa na mchezo wa kesho (leo) ambao nitautumia kujua udhaifu wa timu kabla ya kucheza mechi za kufuzu Afcon,” alisema Kim.

Alisema katika mchezo huo atazingatia zaidi mbinu za kushambulia na kujilinda ili kujiandaa na mechi za kufuzu kwa sababu anaamini zitakuwa na ushindani mkubwa.

Pia alisema wachezaji wengine ambao wana majuku kwenye timu zao watajiunga na timu baada ya mchezo wa kesho na watacheza mchezo wa Machi 18. Taifa Stars itaitumia michezo hiyo kwa ajili ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) dhidi ya Equatorial Guinea utakaochezwa ugenini Machi 25 na dhidi ya Libya, Machi 30 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Taifa Stars ipo Kundi J ikiwa na pointi nne, Tunisia wanaongoza wakiwa na pointi 10, Equatorial Guinea wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi sita na Libya wanashika mkia wakiwa na pointi tatu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2d2549c6fdaeb85bda3167cfd893f659.png

MGOGORO kati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi