loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wamachinga Dodoma wamlilia Magufuli

Wamachinga Dodoma wamlilia Magufuli

WAFANYABIASHARA ndogondogo maarufu kama machinga jijini hapa, wamesema watamkumbuka Rais John Magufuli kwa namna alivyowajengea mazingira mazuri ya kufanya biashara zao.

Wamesema kabla ya kuingia madarakani walikuwa wakifanya kazi zao kwa wasiwasi huku wakiishi kama digidigi, kutokana na namna walivyokuwa wakibighudhiwa na mamlaka mbalimbali.

Akizungumza jana na HabariLEO jijini hapa, Frank Damiano ambaye ni muuza viatu katika Barabara ya Tisa, alisema wamepokea kifo cha Rais Magufuli kwa masikitiko makubwa.

“Vijana tunalia tutampata wapi Rais kama Magufuli, alitutetea sana, tulikuwa tunafanya kazi zetu kwa kudharaulika sana, lakini akatujengea mazingira mazuri ya kufanya kazi zetu na sasa hakuna bughudha tena,” alisema.

Akaongeza: “Unakuja mtaani unafanya biashara unapeleka chakula nyumbani; maisha yanakwenda…” Alisema Rais magufuli amewezesha hata watoto wa maskini kwenda shule baada ya kuanzisha na kutekeleza sera ya elimu bila malipo hali iliyowezesha wengi kuanza na kuendelea na masomo.

“Amejenga reli na miundombinu mingi ambayo inawezesha taifa kusonga mbele kimaendeleo,” alisema.

Wafanyabiashara hao wametengeneza mabango ya maboksi yenye ujumbe wa “Machinga tutakukumbuka daima,” kama njia ya kuenzi mchango alioutoa kuboresha mazingira ya kufanyia biashara.

Naye Shem Hassan, alisema watamkumbuka Rais Magufuli kwa kuwajengea mazingira wezeshi na yenye heshima ya kufanya biashara. “Zamani tulikuwa tunakimbizwa kama digidigi, Rais Magufuli alipoingia madarakani ndipo tukawa na uhuru wa kufanya biashara, ametusaidia sana katika hili hawezi kuondoka kwenye mioyo yetu,” alisema.

Alisema hata katika ofisi za serikali, wananchi wa kawaida sasa wanathaminiwa tofauti na ilivyokuwa zamani kwani sasa hospitalini wananchi wanapata huduma bora tofauti na ilivyokuwa awali walipolazimika kutoa rushwa.

Mkazi wa Dodoma, Alfakisadi Ganyara, alisema kifo hicho kimekuwa cha ghafla na kimeshtua Watanzania wengi.

Alisema atakayerithi mikoba yake, hana budi kuendelea na kasi ya Rais Magufuli ili amalizie kazi iliyobaki.

“Atakayepokea kijiti chake, tumsaidie na tumuombee ili kushirikiana kukamilisha mambo mazuri na miradi mikubwa ya kimkakati aliyoianzisha Rais Magufuli ili ikamilike na kuleta tija kwa

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi