loader
Dstv Habarileo  Mobile
Manonga: Magufuli ni namba moja Afrika uwekaji wa umeme

Manonga: Magufuli ni namba moja Afrika uwekaji wa umeme

MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ambaye pia ni Mbunge wa Manonga, Seif Gulamali amesema Rais John Magufuli aliisaidia nchi kuwa namba moja Afrika katika uwekaji wa umeme.

“Katika sekta ya umeme tuna haki ya kujivunia kwani Rais Magufuli aliwezesha tuwe wa kwanza Afrika katika uwekaji wa umeme. Rais alifanya tuwazidi wenzetu wa Rwanda, Kenya na nchi zetu majirani’’alisema.

Alisema Rais Magufuli atakumbukwa kwa wema wake, upendo wake  pamoja na ujasiri wake.

Kwa upande wake Mbunge wa Chato ambaye pia Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alisema ni pigo kubwa kuondokewa na Rais Magufuli.

“Ni pigo kubwa sana kwangu, Rais Magufuli alinifundisha siasa, ujasiri na kufanya  mamuzi katika utendaji wangu wa kazi,” alisema Kalemani.

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@

 

Kanisa lamuomba Samia kufuata nyayo za Magufuli

Na Veronica Mheta, Arusha

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la International Evangelism lililopo Sakila wilayani Arumeru, Eliud Issangya amemtaka Rais Samia Suluhu Hassan kufuata nyayo za mtangulizi wake, John Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Askofu Mkuu Issangya alisema  ni vema Rais Samia akafuata nyayo za Magufuli ili kuendeleza miradi mbalimbali iliyoanzishwa na mtangulizi wake huyo.

Alisema alifanya  kazi na Magufuli kwa miaka sita, ana maono na lazima maono yake yafuatwe kwa kuendelezwa kwa nguvu na kasi ileile miradi yote inayoendelea hivi sasa nchini kote.

''Iwe katika elimu aendelee na sera ya kutoa elimu bure kwa watoto maskini wa Tanzania au katika afya, ahakikishe hospitali,vituo vya afya na zahanati nyingi zinazojengwa nchini kote zinakamilishwa na nyingine zinajengwa, hiyo itakuwa heshima na urithi wa kudumu kwa Magufuli,"alisema.

Aliongeza kuwa Rais Samia ahakikishe miradi mikubwa ya kimkakati kama ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR, bwawa la kuzalisha umeme la Rufiji, usambazaji wa umeme vijijini ambayo ilikuwa sehemu ya maono aliyoishi nayo, inaendelezwa kwa kasi ileile kwa manufaa mapana ya taifa.

Askofu Mkuu huyo pia alimtaka Rais Samia kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa, kutowavumilia watendaji wabovu serikalini, kuwatetea wanyonge ili kumuenzi Magufuli ambaye anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake Chato mkoa wa Geita wiki hii.

"Tulipokea tangazo kwa kifo cha rais wetu shupavu kwa mshtuko mkubwa na masikitiko mengi, kwa sababu ni tukio limetokea na hatuna la kufanya lakini daima tutamkumbuka kwa mambo mengi aliyotufanyia, kama taifa katika muda mfupi wa uongozi wake,"alisema.

foto
Mwandishi: Alexander Sanga

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi