loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rais Malawi ataka viongozi Afrika kuiga utendaji wa JPM

Rais Malawi ataka viongozi Afrika kuiga utendaji wa JPM

RAIS wa Malawi, Dk Lazarus Chakwera amesema viongozi wa Afrika hawana budi kuiga mfano wa uongozi wa hayati John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17 jijini Dar es Salaam.

Dk Chakwera ameyasema hayo leo mjni Dodoma wakati akitoa salamu zake za rambirambi kufuatia kifo cha Rais John Magufuli.

Alisema misimamo ya hayati rais Magufuli  katika kuiongoza wake nchini,  imeonyesha nchi za Afrika, zinaweza kufikia malengo bila  kufuata matakwa ya taasisi mbalimbali za kifedha, ambazo zimekuwa zikiwaumiza.

Amesema  hivi karibuni, Rais Magufuli alimwandalia chakula Ikulu ya Dar es Salaam na kesho yake, akamsindikiza uwanja wa ndege. “Sikujua kama ilikuwa siku ya mwisho kuona naye na alikuwa akiniaga,” alisema kwa uchungu.

“Waliposema miradi mikubwa ya miundombinu haiwezi kukamilishwa kwa wakati, walimwona Magufuli akifanya. Kila mmoja ameona na hakutaka kufuata maelekezo ya taasisi za kifedha ambazo zimekuwa zikiacha Afrika na madeni makubwa,” amesema Rais Chakwera.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi