loader
Dstv Habarileo  Mobile
Magufuli alipambana na matatizo sugu Afrika- Rais Malawi

Magufuli alipambana na matatizo sugu Afrika- Rais Malawi

Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera amesema Rais Magufuli alifanikiwa kupambana na kuondoa matatizo mengi na makubwa nchini, ambayo awali yalionekana kuwa changamoto zisizoweza kutatuliwa na serikali za nchi barani Afrika.

Amesema miongoni mwa mambo ambayo Rais Magufuli amefanya na hayakutarajiwa, hivyo kuushangaza ulimwengu, ni pamoja na kuondoa uvivu na kuongeza uwajibikaji kazini, kudhibiti rushwa, kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati ndani ya miaka mitano.

Pia amesema kuwa alikamilisha miradi mikubwa ya miundombinu kwa bajeti mwafaka, kutotegemea maeekezo ya taasisi za kifedha za kimataaifa, ambapo maelekezo hayo yamekuwa yakiziacha nchi za Afrika zikiumizwa na madeni makubwa.

Aidha, amesema ambao wamepata fursa ya kumuona Magufuli, ambaye hakuweza kutabirika, na maisha yake ya utumishi wa mfano, watabaki na kumbukumbu yake.   

“Mapenzi ya Rais Magufuli kwa nchi yake itakuwa ndio mwanga katika safari yetu kama waafrika,” amesema  Chakwera.

foto
Mwandishi: Isdory Kitunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi