loader
Dstv Habarileo  Mobile
Majaliwa awashukuru wasanii

Majaliwa awashukuru wasanii

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewashukuru wasanii pamoja na makundi mbalimbali kwa jinsi walivyojitoa kwa kutoa nyimbo za maombolezo katika kipindi hiki cha msiba wa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli.

Hayati Magufuli alifariki dunia Machi 17, mwaka huu katika hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es Salaam.

Majaliwa amesema ingawa maombolezo yatakuwa siku 21, lakini wasanii wamemuhakikishia kuwa wataendelea kutoa nyimbo mbalimbali za maombolezo kwaajili ya hayati Rais Magufuli.

“Naomba niyashukuru makundi mbalimbali hasa wasanii ambao wameendelea kutoa nyimbo za maombolezo katika kipindi hiki,” alisema Majaliwa.

Hadi sasa zaidi ya nyimbo tano zimetungwa na wasanii ambazo ni ‘Asante Magufuli’ ulioimbwa na Nandy, ‘Kifo’ uliotungwa na Rayvanny, ‘Tutaonana Magufuli’ ulioimbwa na Peter Msechu na Pole Mama Samia wa Muumin Mwinjuma.

Nyimbo nyingine ni ‘Lala Salama’ ambao umeimbwa na Tanzania All Stars, ‘Nenda Mpendwa Wetu’ ulioimbwa na Tanzania One Theatre (TOT). 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e9e6f243b096596fbbbaadc3477eb64f.jpeg

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa 

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi