loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mwili wa Rais Magufuli kulala Zanzibar leo

Mwili wa Rais Magufuli kulala Zanzibar leo

WAZIRI Mkuu Kassim, Majaliwa amesema mwili wa Hayati Rais Dk John Magufuli utalala Ikulu Zanzibar leo na kesho utasafirishwa kwenda jijini  Mwanza kwa ndege na baadaye utasafirishwa kwenda Chato.

Majaliwa amesema baada ya mwili kuwasili utapelekwa moja kwa moja katika Uwanja wa CCM Kirumba ambapo misa na dua zitafanyika kuanzia saa 1:00 asubuhi ikiwa ni pamoja na kutoa heshima za mwisho kwa wakazi wa jiji hilo.

Wananchi wa Mkoa huo watapata fursa ya kuaga na baadaye mwili utapitishwa katika Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza kabla ya kuanza safari kupelekwa Chato kwa kupitia daraja kubwa la kisasa lenye urefu wa kilomita tatu, lililopewa jina la Magufuli.

“Baada ya kuvuka katika daraja hilo lililopo Kigongo Busisi mwili utasimama kwa muda i nyumbani kwa mke wa marehemu Busisi  kwa dakika 10 ili wazeee, ndugu wa mke wa marehemu watashuhudia na kupata fursa ya  kumuaga mpendwa wao kisha utaeleka Wilaya ya Sengerema, Geita, Katoro  hadi Chato mji wa Lubambangwe,” alisema Majaliwa

Ameongeza kuwa maandalizi yote muhimu kwa ajili ya taratibu za maziko ya Rais Magufuli zimekamilika na usalama utakuwepo wa kutosha

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi