loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rais Mwinyi: Magufuli aliwajibika 

Rais Mwinyi: Magufuli aliwajibika 

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amemtaja Hayati Dk John Pkombe Magufuli kama kiongozi aliyefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika uwajibikaji kwa watanzania na uadilifu katika jamii.


Dk Mwinyi amebainisha hayo leo katika Uwanja wa Amaan Jijini Unguja kwenye hafla ya kuuaga mwili wa Hayati Dk John Pombe Magufuli kwa wananchi wa Zanzibar.


“Tunamkumbuka kwa namna alivyokuwa anapambana na rushwa, ufisadi, ubadhilifu na uzembe ambapo alipata mafanikio makubwa kwa uthubutu wake huo kwenye kujenga uadilifu katika jamii na uwajibikaji katika utumishi wa umma kwa watu kupenda kuchapa kazi” amesema Dk Hussein Mwinyi.


Aidha, Dk Mwinyi amebainisha kuwa Hayati Magufuli atakumbukwa pia kwa namna alivyotekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika kipindi kifupi cha uongozi wake.

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi