loader
Dstv Habarileo  Mobile
Watu bilioni 3.9 washuhudia kuagwa Rais Magufuli

Watu bilioni 3.9 washuhudia kuagwa Rais Magufuli

Watu  bilioni 3.9 kutoka maeneo mbali mbali duniani, wamefuatilia mazishi ya kitaifa ya Hayati Rais Dk John Magufuli yaliyofanyika Machi 22 mkoani Dodoma.


Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, visiwani Zanzibar leo ambako wananchi wa visiwa hivyo walipata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa Hayati Rais John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17 kwenye hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam.


Jeneza lenye mwili wa Hayati Magufuli limepokelewa na  Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi ambaye ameongoza wananchi wa Zanzibar kumuaga.


 “Jambo hili ni nzito, tumeona jinsi watu walivyoguswa. Hakika kiongozi wetu huyu ameondoka wakati ambapo tunamhitaji zaidi. Tunaiombea nafsi yake ilale pema,” amesema  Majaliwa, kupitia hotuba yake akitoa salamu za pole.


|Aidha Majaliwa ambaye ndio mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu mazishi kitaifa, amevipongeza vyombo vya habari  nchini kwa kuripoti kwa weledi tukio hilo tangu kutangazwa kwa msiba huo.


Jana Machi 22, viongozi mbali mbali  kutoka ndani na n je ya nchi,  wawakilishi wa nchi zinazounda Kanda ya Afrika Mashariki na Bara Afrika wakiwemo marais tisa, Waziri wakuu wawili,  walimuaga Rais  Magufuli katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma wakiongozwa na  Rais  Samia Suluhu Hassan .


Hayati Rais Magufuli alifariki Machi 17, 2021, kutokana na tatizo la umeme wa  moyo. Atazikwa Machi 26, 2021, nyumbani Chato.

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi